Page 117 - Your Guide to University Life
P. 117
Maswala ya Pesa Chuoni
-Vitu kuhusu pesa ambavyo natamani ningevijua nilipokuwa chuoni
-Unaweza kuiongeza, kwa kuanzisha biashara (ya chakula, vocha au yoyote ile itakayokuwa inakuingizia). Chuoni ndio mahali pekee ambapo upo ana kwa ana na wateja, kwahiyo hiyo ni fursa ya kufanya pia biashara.
Pesa iliyopo kwenye mzunguko ndio pesa inayozaa, shida inakuja pale ambapo ubize wa chuo unapofanya wanafunzi washindwe kutoka na kuiweka pesa kwenye mzunguko japo baadhi wanaweza. Ukiwa mjanja sambamba na nature ya chuo utakachoenda na namna ulivyokizoea chuo unaweza ukachukua risky move na ukaaanza kukopesha pesa kwa classmates wako kwa riba ya kawaida mfano 10%, hii sasa inategemeana na uchumi wako pia. Lakini ni biashara ambayo haitakupotezea muda mwingi nje ya chuo na itakupatia faida, kwa mfano itakusaidia ku-save lile bumu utakalopata (hakikisha una maandishi au namna ya kuwadai ambayo inakulinda wewe maana sio wote waaminifu).
-Unaweza kuiweka kwenye fixed account ili izalishe baada ya miezi fulani.
-Unaweza weka akiba kiasi fulani kwa ajili ya maisha baada ya chuo, kama ukiweka akiba 50,000 kwa kila hela itakayoingia ina maana ukimaliza chuo unahela ya kukusaidia hata nauli wakati wa kwenda kuombea kazi.
-Kuna njia maarufu sana ya kutengeneza pesa kwa wanachuo, freelancing, ambayo kwa kifupi ni kupata vikazi
117