Page 118 - Your Guide to University Life
P. 118
vidogo vidogo mtandaoni na kuvifanya kisha unalipwa. Kwa mfano, kuna academic writing, ambayo inahusu kuandikia wanafunzi wa vyuo vya ng’ambo assignments. Ili kupata hizi kazi unatafuta akaunti ya kazi, au mtu aliye na akaunti ambaye atakuwa anakupa kazi. Kama kiingereza chako kiko sawa utajifunza kiasi tu na utakuwa ushaelewa na kuweza kuzifanya. Malipo yake huwa mazuri ingawa inalingana na kiwango cha akaunti yako. Ukishajiunga na shule unawezatengeneza marafiki uulizeulize kama wanafahamu mtu aliye na akaunti ambaye anawezakuchukua akufunze na awe anakupa kazi, maana aghalabu kufungua akaunti mpya huwa ngumu.
-Kazi nyingine za freelancing ni kama kudesign logos, graphics, kutengeneza subtitles, transcription n.k. na hupatikana mitandaoni mfano mtandao wa Fiverr, hivyo unaweza angalia ujaribu, ila ujue, nyingi ya hizi huhitaji training. Habari njema ni kwamba unaweza kujifunza kupitia mitandao – blogs na YouTube na uanze.
Hela utakazopata unaweza kuzitumia kwa matumizi yako binafsi ama ya shule kama pocket money ya mzazi haitoshi, na pia unaweza kuziweka kwenye akiba. Ukishamaliza chuo akiba hii itakusaidia kuanzisha biashara, ama kujiendeleza kwenye kazi uliyosomea, ama pia unaweza kuendelea na freelancing ukingoja kupata kazi, ama hata ukishapata uendelee nayo kama side hustle.
118