Page 120 - Your Guide to University Life
P. 120
Ujuzi wa kidijitali unaoweza kujifunza toka ukiwa chuo unaoweza kukupatia kipato ukiwa chuo au wakati unaendelea kutafuta ajira mtaani au hata kukufanya ujiajiri
Kama nilivyosema hapo mwanzo ni vizuri kuwa na ujuzi mwingine zaidi ya kile unachosomea chuoni, yani jifunze kitu kingine wakati bado upo chuoni ili ukimaliza mkononi unakuwa na cheti na ujuzi wa kitu kingine kinachoweza kukusaidia kupata ajira au kujiajiri.
Kuna vitu kadhaa unavyoweza kujifunza mtandaoni ambavyo ni skills nzuri zenye soko, skills hizo ni kama vile;
--- Graphics Designing
Nawafahamu watu ambao wamesomea mambo mengine kabisa, ila walichukua muda kujifunza graphic designing na wakawa wanafanya majaribio chuoni ili kukuza ujuzi kwa kudesign matangazo ya vikundi vya dini, matangazo ya chuo nk. Wakaja kujiajiri na sasa ni ma-grapics designers maarufu ila walijifunza skill hiyo wakiwa chuo
--- Photography
Stori ya hii inafanana kabisa na hiyo ya graphics designing, namjua mtu aliyejiajiri na ana studio yake ila alianzia chuo na ana cheti cha mambo mengine kabisa
--- Video Editing
--- Content Marketing na mambo ya social media marketing
120