Page 12 - Your Guide to University Life
P. 12
Mawazo 5 unayotakiwa uyaache ili kufanikiwa chuoni
Wakati unaenda chuo na muda wote utakaokuwa chuo ni muhimu kuachana na mawazo haya:
1 – Kusoma huku unawaza kuajiriwa
Ni kweli unaweza kupata ajira, lakini huku ukiwa chuo changamsha akili kidogo unaweza pata jambo jingine tofauti tu na kumaliza chuo kusubiri ajira. Mtaani kumejaa wahitimu wengi wa fani mbalimbali, ni muhimu toka mwanzo kuanza kuwa mbunifu kufikiria options nyingine wakati bado upo chuo.
2 – Ukipata supp semester moja ndio umejiharibia elimu yako yote ya chuo
Ni kweli supp sio nzuri, ila haimaanishi ukipata supp semester moja, future yako yote ya maisha imeharibika au usitilie mkazo kusoma kwenye semester nyingine kwasababu tayari unarudi kurudia mtihani September au muda ambao chuo chako kinafanyisha supp. Hapana, unaweza ukapata supp na maisha yako yakawa hayajaharibika na ukafaulu sana na vizuri semester nyingine.
3 – Chuo ni bata tu
Kuna kozi na semester inaweza kuwa unakula bata jingi kwa vile ya urahisi wake lakini pia unaweza kubalansi muda vizuri na ukala bata chuo ila haimaanishi chuo ni bata, yani kwamba maisha kila eneo na kila siku ni marahisi.
12