Page 11 - Your Guide to University Life
P. 11

tunavyotumia laptop chuo ni kwaajili ya movie. Wengi tulikuwa tunaitumia hivyo.
Kama hauna, kuhusu kusoma hata smartphone unaweza kusomea na nina mifano mingi ya wanafunzi ambao walitumia smartphone tu kusomea na tumemaliza nao.
Kwahiyo isikupe presha sana kama hauna uwezo wa
 kununua kwa sasa, utanunua tu utakapofanikiwa kiuchumi au utakapoona umuhimu wake kwako, usijipe presha kwasababu ya laptop, smartphone inatosha ukiwa na apps zakukusaidia kufanya mahitaji yako ya chuo kwa smartphone.
(Kama hauna laptop, kuna apps za simu ambazo ukiziinstall zinakusaidia kufanikisha mahitaji yako ya kitaaluma kupitia simu yako, bonyeza hapa kujua apps hizo)
-Chuoni hakuna kufeli
Okay, najua huku shuleni tulikuwa ukifeli ndio inaonekana kama mwisho wa dunia na ndio maana supp, carry na disco havionekani kama vikubwa kwasababu havioneshi kukunyima nafasi nyingine tena kama mitihani mikubwa ya vidato.
   Ila usichezee elimu ya chuo kwasababu ‘kufeli’ kwake hakufanani na ulikokuzoea.
   Na hayo ndio mambo niliyoambiwa kuhusu maisha ya chuo, ambayo niliyaona kuwa ya uongo nilipofika chuo.
Najua na wewe ukifika chuo utajionea mwenyewe kuhusu mambo mbalimbali uliyowahi kuambiwa kuhusu chuo.
11
























































































   9   10   11   12   13