Page 13 - Your Guide to University Life
P. 13

4 – Utapata mume au mke chuoni
Chuoni unaenda kusoma hayo mengine ni ya ziada. Ukienda chuo na wazo la kupata mke utajibana sana kwenye kufurahia urafiki mzuri na wakaka au wadada kwasababu kichwani unawaza kila mtu anaweza kuwa ndio mke au mme.
5 – Kwa vile umefika chuo inabidi uwe “wanachuo wanavyokuwa”
Hakuna namna ‘wanachuo wanavyokuwa’, hakuna box la vile unavyobidi uwe kwa vile wewe ni mwanachuo. Kuwa wewe. Jaribu mambo mbalimbali usijibane kwa vile hayaendani na level yako unayohisi umefikia kwa kuwa mwanachuo. Usiishi kwenye box, usiingie gharama za kulilinda hilo box ulilojiweka kwa vile tu sasa umefika chuo, hakuna namna moja ya watu kuwa kwenye maisha, be yourself. Usiangaishwe sana na trends, ishi maisha yako.
13






























































































   11   12   13   14   15