Page 15 - Your Guide to University Life
P. 15
Hisia mbili utakazokuwa nazo unapoenda chuo
Bado nakumbuka siku nilipofika Mbeya tayari kuanza mwaka wangu wa kwanza. Nakumbuka nilivyoamka asubuhi baada ya kuingia Mbeya usiku sana na kulisikia lile baridi ambalo ndio lilienda kuwa sehemu ya maisha yangu kwa miaka minne iliyofuata. Bado nakumbuka nilivyokuwa napelekwa chuo, na tukapita barabara kuelekea geti kuu la chuo cha Mbeya University of Science and Technology, harufu nilizozisikia, vile nilivyojisikia na vitu nilivyoviona.
Siku ile ilikuwa moja ya siku nzuri na ya kukumbukwa kwenye maisha yangu.
Mwezi huu unapokaribia kwenda chuo kwa mara yako ya kwanza na tayari kuanza maisha mapya kwa miaka mitatu/minne/ mitano ijayo, natamani nikushirikishe hisia ambazo unaweza kuzisikia unapoenda chuo kwa mara ya kwanza:
1: Furaha na Matarajio
Unakuwa ‘excited’, maisha mapya unaenda kuyaanza ambayo yatakubadilisha, sasa unakaribia utu uzima. Unaenda hatua mpya. Siunajua vile tukiwa vidato vya chini tunalenga kwenda chuo, na sasa ndio unaelekea huko tulipokuwa tunaota kwenda – chuoni. Lazima utajisikia furaha na matarajio ya maisha yako haya mapya.
Kuna zile hisia mchanganyiko zinakuja kichwani na kujaribu kutengeneza picha kichwani namna chuo patakavyokua, majengo, wanafunzi wake, wahadhiri n.k ni kawaida sana na hata ulichokiwaza ukienda chuo ukakuta sicho wala usiwaze
15