Page 16 - Your Guide to University Life
P. 16

sana na kuanza kukichukia chuo, maana lengo lako kwenye maisha ndio limeandikiwa kutimiziwa hapo.
2: Woga wa Sintofahamu
Haujawahi kuishi hayo maisha hapo kabla, ndio mara yako ya kwanza unaenda chuo, kuwa huru, mbali na marafiki uliowazoea, unaenda kutengeneza marafiki wapya na kusoma masomo mapya na kozi ambayo inaweza ikaongoza kazi utakayofanya maisha yako yote, ushasikia maneno kibao ya kuhusu chuo na vile wahadhiri na maisha ya chuo yalivyo, ni lazima kuogopa.
Unaogopa kwamba labda unaweza ukafeli, unaogopa labda yatakushinda, yatakuwa magumu, unaogopa mengi ambayo unayawaza sasa hivi.
Haya ndio natamani Eunice aliyekuwa anaenda chuoni mwaka 2014 angeyajua – ‘utakuwa salama, ndio, mambo ni magumu au yatakuwa magumu lakini wewe ni mshindi, wewe ni mpiganaji utaweza kuyashinda, utapitia yote ila utamaliza tu, kama ulivyofaulu vidato najua na chuo utafaulu’.
Na hicho ndicho ninachokuambia sasa hivi wewe.
Usiogope kwamba haujui hiyo miaka mitatu au zaidi ijayo itakuwaje, usianze kuogopa. Labda kutokujua ni jambo zuri, kwasababu katika kutokujua kuna mema. Katika kutokujua yote yanawezekana kutokea, mema au mabaya.
Vipi kama usichokijua ni chema na sio kile unachofikiria kuwa kibaya? Kwa vile haujui ina maana kuna uwezekano.
 16


























































































   14   15   16   17   18