Page 18 - Your Guide to University Life
P. 18

Vitu vya kupaki unapoenda chuo / vinavyohitajika kununuliwa mara tu ukifika chuo
Pamoja na fomu ya usajili ambayo imejazwa na vitu vilivyotajwa kwenye hiyo fomu vitakavyokusaidia kwenye usajili kama cheti cha kuzaliwa nk, hivi ni vitu unavyoweza kuvipaki toka nyumbani au ukanunua mapema tu ukifika chuo;
-Ndoo ya kuogea
-Sabuni, ogeo, kidude cha kuwekea sabuni na brush au jiwe,
-Bakuli la chakula, kijiko, osheo na sabuni,
-Mwamvuli
-Chupa ya maji
-Mto wa kulalia (kama unapenda)
-Mashuka
- Pochi / begi la mgongoni la mtoko au darasani
-Godoro (kama hautokaa kwenye mabweni)
-Madaftari
-Begi dogo la kuwekea hela, kadi na vitambulisho
-Earphones (kama utapenda)
-Nguo za kuvaa kukutosha semester au mpaka utakaponunua na nguo za ndani za kutosha
-Nguo za kulalia -Mataulo
  18


















































































   16   17   18   19   20