Page 21 - Your Guide to University Life
P. 21

Vitu 5 vya kutarajia wiki ya kwanza chuoni
1 - Kupotea madarasa na vyumba vya mabweni
Ni kawaida, ndio mara yako ya kwanza hapo chuoni. Kuepuka hili tumia muda kidogo kuzurula chuoni ili ujue/ ukariri maeneo machache, ila hakuna presha una miaka mitatu/ minne au mitano hapo chuoni kwahiyo utazoea tu. Ila ni kawaida kwa wiki ya kwanza kuingia chumba ambacho sio chako usijikie vibaya au aibu, utazoea tu.
2 - Kutokujua kituo
Kama umeenda kusoma mkoa mwingine ni kawaida kabisa kutokujua kituo cha basi, usiogope kuuliza, ni kawaida kabisa kuwa haujakariri alama za kukuonesha wapi unashukia uliza na jitahidi ukariri mapema ili usipitishwe kila siku
3 - Kukutana na watu uliopotezana nao
Unawakumbuka wale marafiki na jamaa uliosoma nao shule ya msingi halafu kila mtu akaenda njia yake? Wengine unaweza kukutana nao chuo. Uliocheza nao utotoni muda mwingine, au uliokuwa nao jeshini/sekondari/ au unaowajua kwa vile mliishi nao mtaa mliohama na familia yako, jiandae kukutana na watu unaowafahamu na marafiki wapya ambao utaanzia kuwafahamu chuoni.
    21



























































































   19   20   21   22   23