Page 23 - Your Guide to University Life
P. 23

Mambo ya kufanya wiki za mwanzo chuoni
- Kuzunguka chuo ili kufahamu sehemu mbalimbali za chuo, ni muhimu pia kuangalia na kuyafahamu madarasa yaliyoorodheshwa kwenye ratiba ya kozi yako
- Kujua kituo na sehemu za muhimu kwako, mfano; duka, soko, canteen nk
- Jiwekee mipango ambayo utapenda kuitimiza kwa semester au kwa muda wako wote utakaokuwepo chuo
- Ukipata tu chumba anza kupanga vitu kwenye kabati lako kabla jumatatu ya masomo haijaanza
- Kuanza kutengeneza urafiki na mnaosoma nao au unaoishi nao karibu. Si lazima atakayekuwa rafiki yako wiki za mwanzo ndio awe rafiki yako milele, ukigundua kuwa hakufai au anaishi maisha ambayo hauyapendi unaruhusiwa kumwacha.
- Tengeneza urafiki na waliokutangulia kwenye kozi yako ili upate past paper kwao, mitihani ya chuo mingi ukisolve past paper unakuwa sehemu nzuri, kwahiyo anza kuzikusanya mapema. Ila pia waliokutangulia wanaweza kuwa msaada mzuri na kukusaidia wewe kujua kozi vizuri na wahadhiri ili usije ukaingia kesi na mhadhiri ambaye sio na ikakuharibia.
 23



























































































   21   22   23   24   25