Page 25 - Your Guide to University Life
P. 25

kuwasilisha mahitaji yako kwa watu wengine lakini pia kusuluhisha ugomvi kati yako na mtu mwingine ni jambo zuri kujifunza mapema. Lakini pia unajifunza kushirikiana na watu katika maisha, katika kuishi pamoja mwengine anaweza umwa au kupata tatizo lolote, kushirikiana na watu na kuishi na watu ni ujuzi mzuri utakaokusaidia hata huko mbele maishani.
- Upweke unapungua kwasababu uko na watu, katika kushirikiana kuna kuamshana ili msome, kuna matani na vitu mbalimbali, unakuwa hauko peke yako hasa kwa wale ambao ni extroverts.
Hasara za kukaa on campus
Kuna hasara kadhaa pia zinazotokana na kukaa hostel, nazo ni;
- Unachelewa kujifunza kujitegemea, kwa wengi hasa waliotoka shule za boarding, kukaa tena hostel wanaweza kuhisi ni kama kukaa tu boarding kama vile hakuna mabadiliko yoyote. Kwa watu hawa kukaa hostel kunaweza kuwa ni jambo zuri kutokana na faida nilizosema lakini pia hili linaweza kuwa jambo baya kwa kuwa watakuwa sio watu wanaoweza kujitegemea au kujua kujitegemea kwa kuishi wenyewe mapema.
 25





























































































   23   24   25   26   27