Page 26 - Your Guide to University Life
P. 26

Kwa sisi tuliomaliza, wengi wanakuwa wepesi kupanga na kuanza maisha mbali na wazazi kama walikuwa wamekaa off campus, sio wote au sio kwamba wanaokaa on campus hawawezi kufanya hili, ila kujitegemea kunakuja kwa urahisi sana kwa watu ambao hawakukaa hostel kwa vile wanajua gharama za maisha, wanajua kukaa peke yao nk.
- Kukosa privacy, kwa wale wanaopenda privacy on campus haipo sana kwa vile wote mpo chumba kimoja kila mtu anaona mambo ya mwenzie nk. Zaidi tu ya kuwa na kabati lako, kuvaa, kula nk ni mambo ambayo sio private tena ukiishi na watu chumbani.
- Ratiba zako zinaweza kuwa ziaenda kwa kushawishiwa na wengine, inawezekana ni mimi tu ila nilikuwa nafarijika nikiona roommate amelala kama tuna mtihani badala ya kujali ratiba zangu naona bora tulale wote maana sipo peke yangu ninayelala. Chuo ni sehemu unayoweza kujitambua wewe ni nani (individuation), kukaa on campus kunaweza kukufanya uwe mwepesi sana kupelekwa na peer pressure kuliko kufikiria wewe mwenyewe kuhusu maisha yako na ratiba zako. Najua watu kadhaa ambao waliingia kwenye mahusiano yasiyowafaa kwa vile vyumba walivyokuwa wanakaa roommates zao walikuwa kwenye mahusiano.
- Kushindwa kula vizuri, mlo kamili. Kama upo on campus na hawaruhusu kupika basi vyakula unavyokula vingi sio mlo kamili kama vile ambavyo ungeandaa mwenyewe ukiwa off campus. Kwa jinsi
26






























































































   24   25   26   27   28