Page 24 - Your Guide to University Life
P. 24
Je ukae hostel za chuo (on campus) au upange (off campus?
Kuna faida na hasara za uamuzi wowote kati ya maamuzi haya mawili, ningependa nikushirikishe yote ili ujue unachagua lipi.
Faida za kukaa ndani ya chuo / hostel za on campus
Faida za kukaa on campus ni pamoja na;
- Kwa vyuo vingi gharama / ada ya hostel iko chini ukilinganisha na kupanga ambapo ukipiga mahesabu ya mwaka mzima gharama inaweza kuwa kubwa.
- Unakuwa karibu na chuo, kipindi cha mitihani haupati shida lakini pia kama mna vipindi vya usiku hautembei usiku sana kwenda sehemu ya mbali au kama una uchovu unaweza kimbia mara moja hostel kulala muda unaosubiria vipindi ukilinganisha na anayekaa off campus ambaye labda kama amepanga mbali ni lazima akatafute usafiri kwenda kwake.
- Zaidi ya chakula na malazi, gharama za maisha zinakuwa chini kidogo lakini pia una muda mwingi wa kuwaza kuhusu masomo na sio mahitaji ya nyumbani ulipopanga kwa mfano maji, umeme nk
- Unajifunza kuishi na watu kwa kuishi na wale utakaopangiwa nao chumba kimoja. Kujua jinsi ya kuishi na watu mbali na familia yako ni ujuzi mzuri kuwa nao, kujua jinsi ya kuwasiliana vizuri na
24