Page 28 - Your Guide to University Life
P. 28

Aina za roommates utakaokutana nao chuo
(Kama haumuoni au hauna unayemfikiria kichwani basi jichunguze inawezekana ni wewe)
Hizi nimeziweka kwa utani tu na kukufanya ujiandae kiakili kukutana na watu wenye tabia mbalimbali, kwasababu watu tunatoka nyumba na maisha tofauti, haimaanishi kuwa uwadharau au uone vile wanavyoishi maisha yao sio sawa, kila mtu anaishi maisha yake kwa kuona kuwa ni sawa kwake kutokana na mambo mbalimbali yanayomfanya afikirie hivyo, heshimu tu vile watu wanaishi kama haikusumbui au haikuingilii maisha yako.
---
Roommates utakaokutana nao chuo ni pamoja na;
-Roommate anayedhani yeye ni mama/baba wa chumba na nyie ni watoto wake
-Hajapangiwa chumba hicho ila yupo chumbani kwenu kila siku
-Hapendi kuongea sana na nyie anajitenga tu na marafiki zake
-Yule anayependa ushirikiano ananunua vitu vya wote kula, wote kunywa, wote kushea
-Roommate anayesahau na kuondoka na funguo kila siku -Roommate anayeongea na simu kila siku usiku kwa sauti
-Roomamate ambaye muda wa kulala anapenda taa zizimwe
 28























































































   26   27   28   29   30