Page 30 - Your Guide to University Life
P. 30

Mambo ya kufanya kama haumpendi / hampatani na roommate wako
Huwa inatokea kama unakaa hostel muda mwingine unakuwa haupatani na roommate wako mmoja au kadhaa.
Nakumbuka nilipofika mwaka wa tatu pia nilipangiwa room ambayo siku ninayohamia nilipoingia na kuwasalimia wachache walijibu, wengine walinuna. Sababu ilikuwa walitaka wakae wachache kile kitanda changu waweke mabegi, sasa mimi kuongezeka kuliwakosesha hiyo fursa na hivyo tukawa sita ambapo kwao walikuwa wanaona ni wengi. Sio makosa yangu ila muda mwingine binadamu wanakuwa hawajui yupi wa kumkasirikia kwenye jambo fulani hivyo wanamkasirikia anayeonekana karibu yao.
Mimi sikusumbuliwa na lile, ila lililonisumbua ni kuwa wakati tunaishi sasa ile chuki ikawa inaonyeshwa kwa namna mbalimbali, mara kukaripiwa, kuelekezwa kitu cha kufanya utafikiri kuna mmoja ni mama mwenye nyumba, maseng’enyo nk
Unaweza kujikuta upo upande ambao haupo vizuri na roommates / roommate wako kwa sababu mbalimbali ila ukijikuta upo katika hilo ni muhimu kujua kuwa chuoni mnakutana watu mliotoka familia mbalimbali na hivyo ni rahisi kuwa na misimamo, tabia au jinsi ya kufanya mambo ambayo ni tofauti. Chuoni unakutana na watu waliopitia mambo mbalimbali hivyo muda mwingine wanakuwa na namna ya kuishi na watu iliyotofauti na wewe.
Ni muhimu pia kujua sio kila kitu au hasira za mtu ni kuhusu wewe au wewe ndio umezisababisha ila hiyo
  30




























































































   28   29   30   31   32