Page 32 - Your Guide to University Life
P. 32

Haupungukiwi popote unapotafuta amani na watu hasa kama ni werevu na wao wanapenda amani.
Lakini kama ni mtu ambaye sio mwerevu au unamuona ni mpenda shari ni heri uweke mipaka tu, chumbani unaenda kulala na una haki ya kuwa hapo kwahiyo kuwa tu na mipaka ya jinsi ya kuishi naye halafu endelea na maisha yako.
- Kwa kina dada unaweza funga khanga kwenye kitanda chako usionekane na wengine
Kwenye kesi kama hii basi wewe ndio utakuwa roommate anayejifunika na khanga ili uendelee na mambo yako, kama unapenda lakini sio lazima.
- Unaweza kuomba uhamishwe chumba kama unaona huo ugomvi unakusumbua au ni mkubwa sana au unakutishia maisha yako kwa namna moja au nyingine.
- Asikukaripie muda mwingine inabidi ujisimamie na kusema kitu, hauko chini yake, wote mpo sawa, mmelipia gharama sawa za chumba.
Jua haki zako hapo chumbani pia, mtu asikupelekeshe, ishi kama una haki ya kuishi kwenye hicho chumba.
Ni muhimu kujua kuwa mara nyingine inatokeaga roommates wako wanakuwa marafiki zako wazuri na wakaribu ila mara nyingine huwa sio hivyo. Sio jambo la kujisikia vibaya kwani si lazima sana roommates wako ndio wawe marafiki zako maana mwaka mwingine wa masomo
32


























































































   30   31   32   33   34