Page 34 - Your Guide to University Life
P. 34
Mambo ya kufanya kama hauna mazoea ya kuishi chumba chenye watu wengi
Kama haujazoea kuishi na watu wengi ni muhimu kujua kuwa ni jambo la kawaida, sio kwamba una roho mbaya nk. Chuoni mnakutana watu mliotoka kwenye maisha na familia tofauti, kuna tabia na mazoea tofauti yanayokuja na kujitokeza mnapokuwa mmetokea familia tofauti. Yani hilo ni jambo la kawaida kabisa.
Kuna mawili, unaweza kupanga; hii itakurahisishia na kukupunguzia hata kuwa bored kwa mambo ambayo watu wengine watakuwa wanafanya, lakini pia unaweza kuishi hostel ila tu inabidi ubadilishe mtazamo kidogo.
Kwanza inabidi ukubali kuwa mnatoka familia tofauti hivyo kuna mambo watu watafanya ambayo ni tofauti na yanavyofanyika familia yenu na vile ungependa yafanyike. Na hii inakuja kwako pia kuna mambo utafanya ambayo ni tofauti na mtu aliyetoka kwenye familia/ mazingira/ mazoea mengine.
Inabidi ukubali kuwa kuna yale unayoyaona mabaya ambayo kwa wengine sio, kuna yale unayoyaona mazuri ambayo kwa wengine sio. Kubali tofauti zenu, kubali kuwa utaishi na watu wengine, utaishi na watu wengi, jiandae kisaikolojia kukutana na hilo.
Pili jua kuwa haupo hapo kubadilisha maisha au tabia za watu. Usije ukawa kama mama/ baba wa chumba hicho mpaka ukaboa wengine, jitahidi kutokuwa mlalamikaji wa kila jambo linalotokea ambalo ni tofauti na vile ambavyo
34