Page 36 - Your Guide to University Life
P. 36

- Jua kua sio kila mtu anapenda kushare vitu, muombe kwanza kabla ya kudhani anapenda kushea
Hii hasa kama ni mara yako ya kwanza kuishi na watu, waangalie kwanza au ongea nao unapotaka kutumia vitu vyao. Sio kila mtu anapenda kushea, sio kila mtu anapenda mwingine awe kwenye mipaka yake, na kwa vile mko tofauti ni vizuri kujua tofauti zenu ili mjue mnaishije nazo.
- Kama wewe sio mtu wa kupenda kuongea sana au kusikia maneno ya wengine basi ukinunua earphone / headphones itakupunguzia kelele za watu wengi.
Mimi ningekushauri ujichanganye ili ufurahie muda wako wa kuishi na watu, upate vyote ikiwemo makelele na maneno mengi lakini pia naelewa kuwa watu wako tofauti hivyo inawezekana unapenda kukaa peke yako au ukimya, earphones zitakuepushia drama nyingi na watu.
- Ni vizuri kujua kuwa kuna watu hawatakupenda na hilo ni jambo la kawaida
Haupangwi chumba kimoja ili mpendane au muwe marafiki, mnapangwa ili muishi pamoja. Jitahidi kuwa na amani na kupendana na wengine ila hata kama ikitokea kuna watu hauwapendi au hawakupendi jitahidi kuishi tu kwa stadi za jamii nao. Jitahidi kuvumiliana. Lengo kuu ni sehemu tu ya kulala.
36




























































































   34   35   36   37   38