Page 38 - Your Guide to University Life
P. 38
zao kwa watu wa nje unaonekana mmbea na pia mwaka mwingine huwezi jua wataishi na mtu yupi uliyewahi kumsimulia na yeye atawaambia mambo gani kati ya yale uliyowasimulia. Ili tu kuwa salama na kutoonekana una tabia za ajabu, ni heri kuwa na wachache unaowaamini kuwashirikisha yanayokukera / unayopitia.
Nahisi unapopitia hili unajifunza kugawanya shida na matatizo, kuna matatizo utakutana nayo sehemu na utakutana na watu wengine ambao hawatajua unapitia hiyo shida ingawa una wengine wachache watakaojua.
Mimi naamini itakuwa tu fursa nzuri kwako kuishi na watu wapya kwa mara ya kwanza, kwangu mimi ilikuwa hivyo na kama itakuwa mbaya sidhani kuwa itakuwa kitu ambacho hauwezi kukimudu. Usiogope. Furahia tu fursa hiyo itakayokusaidia kukua na kujua jinsi ya kuishi na watu wa aina mbalimbali na wenye tabia mbalimbali.
38