Page 39 - Your Guide to University Life
P. 39
Kukaa off campus
Faida za kukaa off campus / nje ya chuo
Njia rahisi ya kujua faida na hasara za kukaa nje ya chuo / off campus inaweza kuwa kuangalia hasara na faida za kukaa on campus, ila kama utapenda maelezo zaidi tuendelee kusoma...
---
Kukaa nje ya chuo / kupanga kuna faida zake nako, nazo ni;
- Unajifunza kujitegemea, unajifunza kuishi peke yako, hii inaweza kukusaidia kujitambua, kujifahamu vizuri, inaweza kukusaidia kwenye individuation, stage ya kujijua wewe kama binadamu ukiwa peke yako mbali na familia na wazazi wako.
Off-campus inakupa exposure ya maisha nje ya notes unazopewa na wahadhiri, inakupitisha kwenye challenges ambazo wenzio watakuja kuzipitia baadae sana. Pia inakuonesha fursa mbalimbali kwa mfano ukikaa off-campus na unamiliki friji ghafla itakujia akili ya namna ya kulitumia friji hilo kukuingiza kipato mfano kutengeneza ice cream na kuuza, au kutengeneza juice na kuuzia watu kitu ambacho mtu wa hostel hawezifanya.
- Unakuwa na privacy, mbali na wapangaji wenzio, unakuwa private na maisha yako. Sio kama ukikaa hostel ambapo maisha yako yanakuwa yamezungukwa na wengine lakini ukikaa off campus unaepukana na roommate wakorofi, unaishi kwa
39