Page 41 - Your Guide to University Life
P. 41
unaweza kaa nje mpaka muda unaoutaka, unaweza karibisha watu chumbani kwako bila kuwaudhi wengine kwa kuwa upo peke yako, unaweza andaa sherehe nk. Lakini pia haugombanii chumba au kuwahi chumba kiasi cha kutoa rushwa wakati unatafuta chumba maana una sehemu yako sio lazima ugombanie hostel ambazo zina vyumba vichache.
Hasara za kukaa off campus
Off campus nako kuna hasara hizi hapa; - Gharama
Mara nyingi kodi, umeme, maji nk ndio vinaweza kuwa gharama na kama unapika basi kuna vyakula, gas, nauli nk. Ukiangalia vyuo vingi gharama ya hostel kwa mwaka ni ndogo kuliko kodi ya mwaka ukipanga sehemu, ila hili linategemeana na chuo na chuo au pia na mkoa uliopo.
- Mawazo ya maisha
Ukishaanza kujitegemea, mawazo na wajibu nao unakuja, mfano boom labda halijatoka au kama hauna boom basi haujatumiwa hela toka nyumbani na mama / baba mwenye nyumba anataka kodi, mawazo haya muda mwingine yanaweza yakaitoa akili kwenye masomo na kukufanya upate hata msongo wa mawazo na usifikirie sana shule kwa kipindi unapopitia tatizo fulani.
41