Page 43 - Your Guide to University Life
P. 43
wewe labda haukucheki WhatsApp na pia jirani yako yupo kozi nyingine na hivyo hajui. Na pia kipindi cha mitihani muda mwingine kuona wengine wanasoma inakusukuma na wewe kusoma, ukiwa peke yako unaweza kujisikia uvivu na ukajitia moyo kuwa uko sahihi hauna haja ya kujisukuma kusoma.
-Usalama mdogo
Tofauti na hostel ambapo mara nyingi kunakuwepo na fensi na walinzi kwa kuhakikisha usalama wa wanafunzi na mali zao, mtaani kwa maana ya off-campus ni nadra kukuta nyumba ina mlinzi na baadhi kukosa fensi kabisa na kuchangamana na raia ambao sio wanafunzi kunakuwepo sana hivyo usalama wa mali na wako binafsi unakuwa ni changamoto kidogo.
Na hizo ndio faida na hasara ninazoziona za kukaa off campus na on campus kama kuna nyingine zozote unazoziona au utakazoziona usisite kunitumia DM Instagram au meseji WhatsApp na kuniambia.
---
Kama utachagua kukaa hostel au utakaa off campus, jua tu sio uamuzi unaoweza kuharibu maisha yako kama vitu vyote viko vizuri yani namaanisha uchumi (unaweza kulipia hiyo sehemu kwa wakati), haikusumbui kwenye masomo, ni sehemu nzuri ya kupumzika na kulaza kichwa chako usiku na maisha yako ya chuo yanaenda kama kawaida. Chagua tu kukaa kule ambapo unapata amani, furaha na uhuru wa kuwa wewe, kama ni on campus au off campus, hizi faida na
43