Page 45 - Your Guide to University Life
P. 45

mtaendana kwa tabia ukizingatia ni marafiki tu, fikiria tu kuwa ndugu yako wa damu pale nyumbani inafika muda mnakorofishana vipi rafiki? Mwisho wa kukaa wawili ndani ya room moja siku zote ni kulumbana na mbaya zaidi mnakua mmenunua vitu vingi kwa pamoja kugawana inakua ngumu.
Kukaa off campus kwa vikundi
Njia nyingine ya kuishi ukiwa chuo ambayo huwa nzuri sana ni kukaa off campus, lakini kwenye vikundi, yaani wewe na classmates wako mnakuwa mnakaa nje ya chuo, lakini mtaa mmoja na mmekaribiana, au hata kupanga vyumba kwenye nyumba/apartment moja. Hili linakupa faida zote za kukaa off campus pamoja na faida kadhaa za kukaa on campus. Unakuwa na uhuru na starehe zako na bado uko karibu na wenzio wa chuo.
Mnaweza kushirikiana pamoja, kusaidiana assignments, kudiscuss kazi za vikundi pamoja na kuwa na nafasi ya kujenga urafiki wa karibu nao. Hasa kama kozi unayoifanya inahitaji uwepo karibu na classmates ili msaidiane (kama vile architecture), njia hii ya kuishi itakuwa nzuri sana.
Ukifika chuo unaweza kukaa kwenye hostel semester au mwaka wa kwanza, muda huo ukifanya urafiki na classmates wenzako. Kama kuna mnaoelewana kabisa unaweza wapa wazo hili au pia unaweza kuta tayari kuna kadhaa wameshapanga vyumba katika mtaa mmoja karibu na chuo. Fanya utafiti wako kuangalia iwapo unaweza kujiunga nao ili kuishi nao kwenye mtaa huo.
 45





























































































   43   44   45   46   47