Page 44 - Your Guide to University Life
P. 44
hasara zikusaidie kufanya maamuzi kama ulikuwa na maswali ya wapi ukae.
Mambo ya kuzingatia ukiwa unatafuta eneo la kupanga
Kama umepanga ukifika chuo ukae off campus au ni jambo unalolifikiria kulifanya basi ni muhimu kufanya maamuzi ya kukaa sehemu nzuri kwako ambayo itakufaa kwenye masomo, usalama wako na maisha ya kijamii, hivyo wakati unatafuta chumba cha kukaa ni lazima uzingatie haya;
-Usalama, ukifika chuo utakuta stori za kila mtaa na sifa zake mahali penye asili ya vibaka au aina yoyote itakayovuruga amani yako usiende
-Mahali ambapo ni karibu na chuo patafaa zaidi
-Mahali ambapo kuna upatikanaji wa huduma za kijamii kama soko, maduka, huduma za kifedha, zahanati, maji ni muhimu sana
-Ukipata nyumba yenye idadi ndogo ya wapangaji itakua vyema zaidi maana itapunguza makelele na migogoro ya hapa na pale maana penye wengi pana mengi.
-Mazingira masafi ni muhimu kuyapa kipaumbele na kama upo vizuri kiuchumi ukipata self-contained room itakua vizuri zaidi sababu maliwato za kushare mara nyingi ni ngumu kuwa safi wakati wote.
-Fanya yote lakini usikae na mtu, ishi mwenyewe na kama lengo ni kupunguza gharama za maisha basi kaa hostel mpaka pale utakapoona kila kitu kipo sawa na uwezo wa kuishi mwenyewe upo. Ni ngumu kupata mtu ambaye
44