Page 42 - Your Guide to University Life
P. 42

- Kuna kausumbufu kakupanda chuo na kushuka
Sio sana ila muda mwingine kama unataka kupumzika tu kidogo kabla ya lecture nyingine inabidi tena ushuke uende kwako, muda mwingine unapanda kwaajili ya discussion tu usiku nk. Ile kupanda na kushuka toka kwako na kwenda lecture rooms ndio inaleta kero. Hasa kipindi cha test, maana kwenye test mtu wa hostel anaweza kuchelewa na bado akawa amewahi ila ukikaa nje ni lazima uhakikishe unatoka muda kabla na ufike chumba cha mtihani kwa wakati au uwahi.
- Unaweza kuwa mpweke kama hauna vitu vingi vya kijamii ambavyo unashiriki
Ujue maisha ya chuo ni kuwa na yale maisha na wenzio, kutoka darasani, kwenda kula, assignment nk. Ukiwa tu unatoka darasani na moja kwa moja unaenda kwako, unakosa ile experience ya kuwa mwanachuo kwa kiasi fulani, unakuwa kama mfanyakazi anayesoma chuo, hivyo kama utakaa off campus jitahidi sana kushiriki kwenye matukio yanayoendelea chuoni.
Jitahidi kuwa karibu na wengine ili pia usijisikie upweke. Jitahidi kuwakaribisha labda nyumbani ili usiishi kipeke yako peke yako na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa mpweke.
- Unaweza usijue ratiba za chuo kama hauko vizuri kufuatilia
Unapoishi na watu hostel ni rahisi kuuliza kama kuna mabadiliko yoyote, ukikaa off campus na ukawa sio mfuatiliaji unaweza ukakuta huku juu wameitwa test halafu
42



























































































   40   41   42   43   44