Page 40 - Your Guide to University Life
P. 40
amani bila magomvi na watu labda wapangaji wenzio.
- Unaweza kula mlo mzuri kama unapika, tena unakula kutegemeana na mood yako mwenyewe badala ya kula tu chochote kinachopatikana canteen.
- Una kitanda kikubwa, kizuri na hauna kelele / purukushani au mwingiliano na maisha ya watu. Hii inaweza ikaendana na ile pointi ya kuwa una-privacy lakini kupanga kuna kufanya uwe na maisha yako, hauna haja ya kushea au kugombana na watu kwa vile wanavyoishi maisha yao inakuwa sio usumbufu kwako.
Huna haja ya kuomba watu wazime taa unapotaka kulala wakati wao wanataka kusoma muda huo, zaidi ya wewe mwenyewe hakuna mtu wa kuongea na simu na kukusumbua muda unaotaka kupumzika. Unaishi kwa ratiba zako na kufanya mambo yako na majukumu yako, kiufupi unaanza maisha ya kujitegemea mwenyewe.
- Hauna masharti mengi yanayokubana na hauna haja ya kuhangaika sana kugombania vyumba na muda mwingine kutoa rushwa ili upate chumba.
Kukaa kwenye hostel za chuo kuna masharti mengi sana yanayokubana lakini pia muda mwingine mnaishi wengi sana kwenye chumba kimoja. Hostel za chuo inakuwa tu kama wale waliopo boarding, masharti, ulinzi na mali za watu ambazo utawajibika kwazo. Ukipanga unaweza kuwa unaishi kwa masharti yako mwenyewe unayojipangia,
40