Page 46 - Your Guide to University Life
P. 46

Aina za classmates utakaokutana nao chuo
(Kama haumuoni au hauna unayemfikiria kichwani basi jichunguze inawezekana ni wewe)
Hizi nimeziweka kwa utani tu na kukufanya ujiandae kiakili kukutana na watu wenye tabia mbalimbali, kwasababu watu tunatoka nyumba na maisha tofauti, haimaanishi kuwa uwadharau au uone vile wanavyoishi maisha yao sio sawa, kila mtu anaishi maisha yake kwa kuona kuwa ni sawa kwake kutokana na mambo mbalimbali yanayomfanya afikirie hivyo, heshimu tu vile watu wanaishi kama haikusumbui au haikuingilii maisha yako.
---
Classmate unaoweza kukutana nao chuoni ni pamoja na;
-Jamaa anaelala kabisa class, sio kusinzia, jamaa analala
-Jamaa ambaye amekuja kusoma sio kutafuta marafiki haongei na watu kabisa
-Kipanga mwenye roho nzuri yani yeye ni rafiki wa kila mtu
-Doja, yani yeye anazugazuga tu mpaka nyie mnashangaa anafaulu vipi
-Jamaa anayejipendekeza kwa wahadhiri sana, ni sahihi kuwaomba wahadhiri msaada ila huyu anadhani kujipendeeza kwa wahadhiri kutamsaidia kwa vile chuoni malecturer ndio wanaobeba maksi zako
-Mr Chuo, yeye kaja kupendeza chuoni hadi kipindi cha mitihani yuko vizuri
-Miss Chuo, yani yeye kaja kupendeza chuoni
 46






















































































   44   45   46   47   48