Page 48 - Your Guide to University Life
P. 48

Vitu ambavyo wahadhiri hawatakufundisha ila inabidi ujifunze mapema ukiwa chuo
Kuna vitu vingi ambavyo chuo kinaweza kukufundisha hasa kwenye kozi unayoisomea. Chuo pia, japokuwa sio moja kwa moja kwa mfumo wa lectures, unaweza kupata maendeleo binafsi, unaweza kujifunza jinsi ya kufanya kazi na timu nk. Kwa kuongezea na hayo kuna hivi vitu vingine ambavyo ni muhimu kujifunza unapokua mtu mzima kwenye jamii ingawa hii elimu haitolewi na chuo ila unaweza kujifunza ukiwa chuo.
Hii ni elimu yako binafsi kama utapenda kuwa mtu mzima anayejielewa au anayeweza kuishi mazingira yoyote, vitu hivi ni vya msingi kuwa navyo, vitu hivyo ni;
- Kujiamini
- Kubadilika kutokana na mazingira (kuweza kuishi
mazingira yoyote na watu wowote)
- Kuacha woga
- Kupanga na kutimiza malengo yako
- Kubadilisha mtazamo unapozidi kujifunza mambo lakini pia kuwa na mtazamo chanya hata unapopitia magumu
- Kujali afya yako ya akili na kujali afya yako ya mwili, nafsi na roho
  48
























































































   46   47   48   49   50