Page 37 - Your Guide to University Life
P. 37

- Usijitenge sana na roommates
Jitahidi kushirikiana nao, wanapokushirikisha jambo. Kama ndio unajifunza kuishi nao, jitahidi tu kuwa mstari wa mbele na kuwaonesha upendo.
Usijitenge hata kama umeamua kutoshirikiana nao isiwe kama uadui fulani, au kuwaonesha kwamba wao wako vibaya au chini yako au wewe ni bora zaidi yao. Ishi tu kawaida.
- Usiwaseme wenzio vibaya nje
Najua utapata mengi sana ya kulalamika kwa vile haujazoea kuishi na watu lakini pia kwa vile nyie ni tofauti na mnaishi kitofauti na vile ulivyozoea, ila jitahidi kuwafanyia vile ambavyo ungependa na wewe ufanyiwe, najua haupendi shida, mapungufu, utofauti au matatizo yako yawe lawama mtu mwingine anazoziongea huko nje.
Hii ni mbaya kwasababu inawezekana ni kweli kafanya hayo mambo ila usipomwambia ukaenda kusema tu nje inakuwa ni kumchafua / kumsema vibaya kwa watu ila pia unakuwa haumpi nafasi ya kubadilika kama vile ambavyo ungemwambia yeye mwenyewe.
Lakini pia kulalamika huku hasa ikiwa kila siku kunawaonesha wale wa nje kuwa labda wewe una chuki au unawadharau hao watu unaoishi nao lakini pia itawafanya watu wawe-bored kukusikiliza stori zako za lawama za chumba chenu kila siku.
Na jambo lingine la mwisho, kwako inaweza kuwa sawa na una haki zote kwa vile umekosewa ila kwa kusema shida
37


























































































   35   36   37   38   39