Page 35 - Your Guide to University Life
P. 35

umezoea mambo kufanywa, penye wengi kuna mengi, mengine yapotezee, fanya yako.
Tatu kuwa mtu ambaye yuko wazi kujifunza, kama haujawahi kuishi na watu itumie hiyo fursa kufanya hivyo.
Ukweli ni kuwa mimi nimetokea kwenye familia ambayo ni mtoto wa pekee na sijawahi soma shule ya boarding hapo kabla, jeshini na chuo ndio ilikuwa kama wakati wangu wa kwanza kuishi mazingira kama ya boarding au ya watu wengi kihivyo. Hili jambo la kuchukulia experience hizo kama sehemu za kujifunza lilinisaidia sana kwenye kujifunza kuishi na watu lakini pia kufurahia wakati huo niliokuwa naishi na watu.
Ichukulie kama nafasi ya kujifunza na kupata maendeleo binafsi ya kitabia na ujuzi, utajifunza mawasiliano, jinsi ya kuishi na watu kipindi cha ugomvi / kuishi na watu wagumu, utajifunza kuishi na watu mbalimbali na jinsi ya kuwepo timu moja na watu tofauti na kuendana nao. Hayo ndio niliyojifunza, najua na wewe ukienda kwa nia ya kujifunza kama utakaa on campus basi utajifunza mengi zaidi ya hayo niliyojifunza mimi nilipoishi na watu chuoni. Chuoni unajifunza mengi sana zaidi tu ya mambo ya darasani, unajiifunza pia kuishi kwenye jamii.
Baada ya kujua hayo, haya mambo yanaweza kukusaidia ukiwa unaishi na watu wengi wakati haujazoea chumba cha watu wengi;
35





























































































   33   34   35   36   37