Page 31 - Your Guide to University Life
P. 31
haimaanishi hautakiwi kujiuliza maswali na kujiangalia kama kuna namna yoyote unayoweza kuwa umechangia au kujaribu kutafuta jambo unaloweza kujifunza kwenye hiyo experience. Kujiuliza ndio njia utakayojua kuwa hiyo hasira yake sio yako ila hana wakumkasirikia na wewe ndio upo karibu.
Lakini pia kwa kupangiwa room fulani, una haki zote za kuwa kwenye chumba hicho kwahiyo usije ukahisi hauna haki ya kuishi au unastahili kufanyiwa mambo ya ajabu kwa vile kuna mtu hakupendi, unahaki ya kuwepo chumbani hapo, na hostel hakuna mzazi wa kukupelekesha zaidi ya matron.
Mambo machache yanayoweza kukusaidia unapoishi room na mtu asiyekupenda au ambaye haupatani naye;
- Nunua earphone / headphones
Hasa kama ana maneno au makelele au analeta watu ambao wanazidi kukusumbua kwa maneno yao. Mimi nilishawahi kaaga room ya watu wanaoongelea wenzao kila kukicha, earphones zinasaidia kujiepusha na kelele au maneno usiyotaka kuyasikia lakini pia kufocus kwenye kufanya mambo yako.
- Ongea naye kama mnaweza kusuluhisha jambo au muwe na mipaka
Muda mwingine unaeza kuta umegombana na roommate ambaye ni mwerevu ambaye mkikaa chini kuongea kuhusu ugomvi yanaisha. Ukiona upo kwenye hali kama hiyo, tafuta amani naye hata kama ni kwa kujishusha ili mpatane.
31