Page 55 - Your Guide to University Life
P. 55
Supplementary, Carry Na Disco. Supp
Bado nakumbuka mara yangu ya kwanza kupata supplementary, ilikuwa semester ya kwanza ya mwaka wa tatu, na niliandikiwa supp katika lile somo na fail katika overall results, nikukumbushe tu ndio mara ya kwanza mimi kuona maneno hayo yameandikwa kenye matokeo yangu.
Nilipigwa na butwaa mpaka nikahisi kuishiwa nguvu, nilikuwa nalala deka la juu na nilikua nimeangalia matokeo kwenye simu hivyo nilikuwa nimelala tu pale kitandani mwili hauna nguvu maana nilijua ndio mwisho nimefeli chuo. Nilihisi kama umeme umepita kutoka kichwani mpaka miguuni, ile ‘fail’ ndio ilinichanganya.
Nilianza kujilaumu kwanini nimecheza ingawa sio kweli, nilijilaumu, nikajiona sina akili, nikaamua kumpigia rafiki yangu mmoja ambaye ni mjuzi kidogo wa supp, nikamuuliza ukipata supp inaandikwaje kwenye matokeo, akanielezea, nikamuuliza inaandikwa na ‘fail’ akasema ndio, inakuwa pass kama umepass yote ila ukiwa na supp wanaandika fail kwenye overall, ndipo hapo moyo ukatulia.
Ila nilijihisi mjinga wiki nzima, sikuwa na moyo wa kusoma semester ya pili kwa nguvu kama niliyokuwa nayo semester ya kwanza, sikuwa na motisha tena, sikuwa na kitu cha kuogopa maana kama September nilikuwa narudi. (Natamani nisingefikiria hivi, ningeifikiria tu GPA yangu ila nahisi ile supp ilinivunja moyo vibaya ndio maana nilikuwa hivi)
55