Page 56 - Your Guide to University Life
P. 56

Niliingia darasani siku inayofuatia ambayo ilikuwa jumatatu, wiki chache baada ya kuanza semester ya pili na nikawa bado nawaza kuhusu ile supp. Nimepata supp nne katika course yangu iliyochukua miaka minne, moja kila semester katika mwaka wa tatu na wanne, ila woga wa supp ulikuwa unaondoka semester ya pili kwasababu tayari unajua hata matokeo yakiwaje unarudi tu kwenye September conference so haina haja ya kuwaza sana.
Sijui ni kitu gani kuhusu supp ambacho kinatutisha au kinatufanya tujisikie vibaya, ila nahisi ile kurudi wakati wenzio wanamalizia likizo, kwamba wazazi wanajua haukufanya vizuri ule mtihani inabidi ukaurudie, au kwamba unapofanya mtihani wa supp usipofanya vizuri, unaweza ukalirudia tena somo (carry).
Natamani ningeambiwa kwamba mimi sio mjinga kwasababu nimepata supp japo kuwa kwenye matokeo imeandikwa fail, natamani ningeambiwa hivyo. Maana nisingejisikia mshtuko ule uliokuwepo kwangu maana semester nzima ya pili sikuwa vizuri. Ningejua hilo ningechukulia supp kama nafasi ya pili ya kujaribu tena kwenye masomo yangu na sio kujihisi kuwa mimi mjinga kuliko wengine darasani.
Ni hivi, kila mtu ana njia yake ya maisha, kuwepo chuo na kutopata supp na kuwepo chuo na kupata supp ni njia mbalimbali, moja sio bora zaidi ya nyingine, kuna vitu mbalimbali ambavyo vinafanya mtu apate supp, muda mwingine wahadhiri wenye roho mbaya, muda mwingine binti kumkataa mhadhiri, muda mwingine ni kuwa hilo somo haupo vizuri tu nk. Kwahiyo kama ukiwa
56






























































































   54   55   56   57   58