Page 58 - Your Guide to University Life
P. 58

(kutoendelea na masomo, mpaka baada ya kipindi cha muda fulani).
Unaweza disco kwa sababu mbalimbali, kuibia kwenye mitihani na kukamatwa, vyuo vingine ukifeli supp au ukiwa chini ya GPA (Grade point Average) fulani (chuo changu ilikuwa 2.0) na sababu zingine mbalimbali. Sitaki kukutisha ila ni vizuri kujua kuwa haya mambo yapo na hivyo jitahidi ili uyaepuke. Ishi tu ukifuata sheria, kuwa mwaminifu kwenye mitihani na kaza kwenye kusoma.
Ushauri Wangu: Kuwa makini na masomo yako. Kama kitu hujui waulize wenzio au kamuulize mhadhiri. Weka jitihada kwenye masomo, wengi huacha kuweka jitihada wakifika chuo kwasababu wanaona ndio muda wa kupumzika, lakini GPA yako na ujuzi unaoupata chuo una maana, soma kwa nguvu na shiriki mambo yako ya kitaaluma vizuri.
(Kama unapenda jinsi ya kupata GPA kubwa ukiwa chuoni, bonyeza hapa kupata dondoo za jinsi ya kufanya hivyo)
   58






























































































   56   57   58   59   60