Page 57 - Your Guide to University Life
P. 57
chuo na haujapata supp, wewe sio T.O na ukiwa chuo na ukapata supp, wewe sio mjinga.
Carry
Huwa nahisi sina haki ya kuongelea vitu ambavyo mimi sijavipitia, marafiki zangu wawili walikuwa na carry, ila mimi sijawahi kuipata nilipokuwa chuo.
Ila hata hivyo napenda ujue kuwa ku- carry somo hakumaanishi wewe ni mjinga, kuna kupa nafasi ya wewe kusoma tena lile somo kwa undani, na kulijua vizuri.
Rafiki yangu mmoja aliewahi kuwa na carry alifanya vizuri carry yake mpaka mwalimu akamuita kwa mshangao wa jinsi alivyofaulu vizuri. Na alisoma vizuri mwaka wa mwisho mpaka hakupata supp kabisa, wakati miaka yote alipata.
(Najua kuwa kuna vyuo viko tofauti likija kwenye swala la carry, kwahiyo ni vizuri kujua ukipata carry kwenye chuo chako hali ikoje na jambo gani linaweza sababisha upate carry. Huu ni mfano tu wa vile chuo chetu kilivyokuwa)
Disco
Najua naongelea vitu vikubwa sana katika maisha ya chuo, kwasababu vinaweza kubadilisha maisha yako ukiwa chuoni, nimeona watu wa karibu wawili waki-disco kwenye maisha yangu ya chuo, mmoja tulikuwa naye mwaka mmoja, mmoja alikuwa rafiki wa rafiki yangu. Nikisema disco namaanisha ku-discontinue
57