Page 59 - Your Guide to University Life
P. 59
Walimu wasumbufu
‘Humu mpo wengi sana wote hamuwezi faulu somo langu’
-Maneno ambayo mwalimu msumbufu aliyasema nilipokuwa mwaka wa tatu alipoingia kipindi chake cha kwanza darasani kwetu.
Nikisema walimu wasumbufu hapa naongelea wale walimu ambao wanafanya tu roho mbaya, hata kama umefaulu wanakuwa na roho mbaya na wanajulikana kwa roho mbaya yao.
Mpaka hapo ulipofika na uhakika ushajua na kujifunza kuwa kwenye maisha sio watu watakupenda au watakuwa wakarimu kwako au watafanya vitu ‘fair’ kwa wote, watu wengine ni tabia yao kutokana na roho zao (au matatizo kwenye maisha yao) kufanya maisha yawe magumu kwaajili ya watu wengine.
Mara nyingi huwa najitahidi kuwaelewa watu, napenda sana kujua kwanini watu wanafanya mambo wanayoyafanya, huwa naona hili linanisaidia kuwaelewa lakini pia kutokuchukulia fujo zao kama ni makosa yangu (sizichukulii binafsi sana) na hivyo likija swala la walimu wasumbufu hizi ndio nahisi sababu zinazowafanya wao wawe vile walivyo;
-Sifa na umaarufu, ni rahisi sana hawa walimu wabaya kuwa wanajulikana kwasababu wanachukiwa, wengi hupenda huu umaarufu hivyo hawajali kuwa ni umaarufu unaokuja kwa sababu ya kuwachukia, wanachojali ni kuwa wanaogopwa hivyo kwao wanaitafsiri kama nguvu, heshima na umaarufu.
59