Page 60 - Your Guide to University Life
P. 60

-Kisasi, labda na wao wamekutana na walimu wakorofi/ wasumbufu wakati wanasoma. Hivyo ule uchungu na hasira kwa waliyoyapitia wanataka na wengine pia wapitie magumu mikononi mwao kama kisasi au kwa vile labda hawajui jambo tofauti na hilo (hawajui njia tofauti ya kufundisha zaidi ya vile walivyofundishwa / fanyiwa wao).
-Matatizo ya kisaikolojia, japokuwa kisasi ni tatizo la kushindwa kusamehe na kuachilia, ila kwenye hili naongelea ukuaji wake, naongelea maumivu ya huyo mwalimu (kama binadamu) anayokuwa ameyabeba toka zamani. Hapa naongelea matatizo kwenye familia yanayoharibu saikolojia yake na kumfanya awe na roho mbaya, hauwezi jua jambo ambalo mtu anapitia, hata walimu wakorofi pia hatuwezi jua wanapitia mambo gani kwenye maisha yao.
Lakini hii haimaanishi kuwa ana haki ya kukufanyia roho mbaya kutokana na matatizo yake au chochote kile, au unastahili yale anayokufanyia na unatakiwa uvumilie kwa vile unaelewa hali anayopitia, hapana. Si sahihi wanayoyafanya ila kwa vile bado yeye ndio ana nguvu kwenye somo lake inabidi tu ujifunze jinsi ya kudili nao ili ukorofi wao usikuathiri.
Jinsi ya kudili na walimu wakorofi ili usiingie kwenye kumi na nane zao
-Nenda kwenye vipindi vyao, mara nyingi wanakuwaga na IQ kubwa wanajua majina ya wanafunzi wote na sura zao.
Ukienda kwenye kipindi haumpi nafasi ya kukutafutia sababu.
  60




























































































   58   59   60   61   62