Page 62 - Your Guide to University Life
P. 62
Aina za watu utakaokutana nao kwenye group la assignment
(Kama haumuoni au hauna unayemfikiria kichwani basi jichunguze inawezekana ni wewe)
Hizi nimeziweka kwa utani tu na kukufanya ujiandae kiakili kukutana na watu wenye tabia mbalimbali, kwasababu watu tunatoka nyumba na maisha tofauti, haimaanishi kuwa uwadharau au uone vile wanavyoishi maisha yao sio sawa, kila mtu anaishi maisha yake kwa kuona kuwa ni sawa kwake kutokana na mambo mbalimbali yanayomfanya afikirie hivyo, heshimu tu vile watu wanaishi kama haikusumbui au haikuingilii maisha yako.
--- -Jamaa anayetegea kazi
-Jamaa anayefanya kazi zote kila siku
-Jamaa anayelalamika kwanini hamshirikiani
-Jamaa anayependa tu kupresent kazi hapendi kufanya
-Jamaa ambaye yuko radhi atoe hela yote yaende vizuri kuliko kwenda kupresent
-Jamaa anayejipa cheo cha uenyekiti
-Jamaa ambaye yuko radhi atoe hela yoyote ile ili kazi asifanye
-Jamaa ambaye mkipanga muda wa kukutana yeye mkimuuliza yuko wapi anasema yuko mjini au mbali na chuo
62