Page 64 - Your Guide to University Life
P. 64
Jinsi ya kupata uwiano (kubalance masomo na maisha ya kawaida au biashara kama utafanya)
Muda mwingine inaonekana kama vile masomo yanakukaba kooni, una assignment 3, test mbili lakini pia kumbuka wewe ni binadamu unahitaji kupumzika au una biashara au una mahusiano yanaokuletea mawazo. Chuoni muda mwingine kupangilia muda ni vigumu maana ratiba unakuta imeshapangwa muda mwingine hadi jioni una masomo au mhadhiri anabadilisha muda kutokana na ratiba zake mwenyewe nk. Kwahiyo kuna semester hauna muda mwingi wa kupumzika kwa vile jinsi ratiba inavyobana.
Lakini katika yote haya ni muhimu kuwa na uwiano kwaajili ya afya yako ya akili maana mambo yakiwa yanaenda shaghalabaghala, ratiba hazieleweki unaweza hisi kuchanganyikiwa lakini pia kama binadamu kuwa na routine na mapumziko kunatusaidia kwa vile sisi sio mashine.
Vitu ambavyo vilikuwa vinanisaidia kuwa na uwiano nilipokuwa chuo ni;
- Kujua kuwa uwiano unaonekana kwa utofauti katika vipindi tofauti
Muda mwingine inaweza kuwa uwiano unaweza upata kwa kuacha yote uangalie shule kwanza halafu kipindi cha kubanwa kikipita ule bata.
Muda mwingine inaweza kuwa kupunguza kulala kwa muda ili uweze kufanya yote (jambo ambalo muda mwingine lina athari).
64