Page 66 - Your Guide to University Life
P. 66
Hata ikija kwenye biashara, ni muhimu kujua kuwa biashara ni nzuri ila wewe sio mfanyabiashara unayesoma, wewe ni mwanachuo unayefanya biashara. Hii pia ipo katika dini, ukiwa sio tena mwanachuo baada ya kufeli / kudisco hauwezi tena kuwa kiongozi wa dini au kuendesha biashara yako maeneo hayo. Kwahiyo ishi na enenda kama mwanachuo mwenye biashara au mwanachuo anayeongoza kikundi cha dini.
- Muda mwigine uwiano unakuja kwa kushirikiana na watu vizuri
Muda mwingine unakuta upo kwenye biashara lakini ndio muda wa kudiscuss assignment, kama unaushirikiano mzuri na watu wa kwenye group lenu wanaweza kufanya na kuandika jina lako na kukusamehe kwa kutokushiriki. Hili pia lipo hata kwenye roommates kukufanyia biashara, kama hauishi nao vizuri hawawezi kukufanyia.
- Muda mwingine uwiano unakuja kwa kufanya mambo yanayokurahisishia maisha kwenye upande mmoja ili uwe na nguvu ya kutosha kwaajili ya upande mwingine.
Mfano unaweza kupanga nguo za kuvaa kwa wiki nzima, ili kwa wiki hiyo muda wa kuchagua nguo na kunyoosha uutumie kulala. Unaweza kupanga zamu na wanaroom ya kwenda kununua chakula kwa wiki kama unakaa hostel ili wiki hiyo ambayo sio zamu yako utumie muda wa kutafuta chakula kufanya mambo mengine. Kuna njia nyingi za kurahisisha maisha na kukupunguzia mzigo wa mambo ya kufanya ukiwa chuo.
66