Page 65 - Your Guide to University Life
P. 65
Muda mwingine uwiano unakuja kwa kutumia muda vizuri ule wa katikati unaokuwa hauna vipindi kufanya yale unayoyapanga na kuwa makini na kuyafanya mambo yako kwa wakati.
- Muda mwingine uwiano unakuja kwa kuomba msaada kwa watu
Hasa kama una biashara hostel ya chuo, unaweza kuwaomba roommates wakuuzie unapokuwa haupo na hivyo ukafanikiwa kupata hela huku unahudhuria darasani. Lakini pia unaweza kuomba msaada kwa watu kukuelekeza kama kuna lecture haukuenda nk. Muda mwingine uwiano huu unaweza kuja kwa kuajiri mtu wa kukuuzia kwenye biashara ili wewe usikose masomo.
- Uwiano pia unaweza kuja kwa kusema hapana kwa mambo mengine au kuja kulipizia kuyafanya hayo mambo mengine baadae
Najua ukiwa chuo hasa umri huu wa ujana tunaendeshwa sana na kujisikia kama vile tuko nyuma au tumeachwa, wengi wetu tunafanya vitu ili tusionekane washamba kwa kutokufanya, lakini pia tunahisi maisha yetu hayako sawa kwa vile hatufanyi yale ambayo yanatrend kwa watu wa umri wetu.
Kwahiyo unakuta tunapenda kwenda kila sherehe ili tusipitwe au tusikose kila kitakachotokea kwenye hiyo sherehe. Ni vizuri kuwa na mambo ya kijamii unayofanya zaidi ya kusoma tu, lakini muda mwingine uwiano ni kujua kuwa hauwezi kufanya yote, au hii sherehe inabidi uiache ikupite.
65