Page 61 - Your Guide to University Life
P. 61

Kwenda darasani pia ni jambo ninalokushauri kulifanya hata kama mwalimu sio msumbufu, mimi kuna supp mbili nilipata chuoni zilitokana na kudoji.
-Kaa mbali na kuwasema sema, mara nyingi wana wanafunzi ambao wameshaenda kujipendekeza kwao, kwahiyo hao huwa wapelelezi wao.
-Fanya wajibu wako kwao kisheria, kama ni assignment ipeleke nk, fanya yale unayotakiwa kuyafanya kwenye somo lao kikamilifu bila matatizo.
-Pia usijipendekeze, jitahidi kutojiweka mbele sana au kujipendekeza kwao. Tulikuwaga na mwalimu mmoja mkorofi ambaye alikuwa hajali umejipendekeza au lah, tena alimpa supp hadi mtu aliyekuwa mpelelezi wake.
Wewe fanya yako, usiogope, fanya wajibu wako kikamilifu bila woga. Uzuri wa matatizo ya chuo ni kuwa hata kama semester hii unahisi hili tatizo haliwezi isha ni kubwa kupitiliza, semester hii itaisha na mpya itakuja na mambo mengine. Kwa hiyo hata walimu wakorofi huwa mnaachana nao semester nyingine au anapewa somo jingine kama mtaendelea naye. Cha msingi tu nasisitiza usiwaogope, ukiwaogopa, ufahamu wako unashindwa kujaji vitu vizuri akihusika yule mwalimu, unaweza hata kupoteza kujiamini kwasababu yake. Kwahiyo hakikisha hauendeshwi na woga wa kumuogopa yeye, yeye sio mungu.
61





























































































   59   60   61   62   63