Page 51 - Your Guide to University Life
P. 51
- Kujipenda na kujipa furaha na kujua vitu gani vinakupa furaha
- Kusikiliza hisia zako unapojisikia vibaya kuhusu jambo fulani na kujua kwanini unajisikia vibaya na kutatua hisia hizo / jambo hilo
- Kufuata ratiba zako na sio za wengine au kupelekeshwa na mambo ya wengine
- Kujua kudhibiti utumiaji wa mambo mbalimbali mfano mitandao ya kijamii, pombe, simu nk
- Negotiations
- Jinsi ya kutatua matatizo, kujichunguza na kujiambia ukweli unapokosea na kujifunza kutokana na makosa
- Jinsi ya kujua na kutambua utapeli hasa wa kifedha au kazi
- Kuongea na watu kwa ajili ya mambo ya kikazi (socializing and networking)
- Kuuliza maswali (kutokuamini kila kitu kirahisi)
- Kuweza kuishi na kusikiliza maoni ya wengine kwa utulivu hata kama haukubaliani nayo na kuweza kuwasilisha yako bila hiyo hali kugeuka kuwa ugomvi
51