Page 6 - SWAHILI_SB01Creation
P. 6

Mungu akasema, "Maji yaliyo chini ya mbingu
        na yakusanyike mahali pamoja, udongo
        mkavu uonekane."
              Ikawa hivyo. Mungu akauita ule udongo
              mkavu, Nchi; na makusanyiko ya maji
              akayaita Bahari.
                      Na Mungu akaona ya
                      kuwa ni vyema.
              Mungu akasema, "Nchi na itoe majani, miche itoayo
              mbegu, na miti ya matunda izaayo matunda kwa jinsi
              yake, ambayo mbegu zake zimo ndani yake, juu ya
              nchi,"  ikawa hivyo.























































                                                                                                                                                               Nchi ikatoa majani, miche itoayo mbegu kwa
                                                                                                                                                               jinsi yake, na miti izaayo matunda, ambao
                                                                                                                                                               mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake.

                                                                                                                                                                             Mungu akaona ya kuwa
                                                                                                                                                                             ni vyema.

                                                                                                                                                                       Ikawa jioni na baadaye asubuhi,
                                                                                                                                                                       siku ya tatu.

                                                                                                                                                                                   Mwanzo 1:9-13
   1   2   3   4   5   6   7   8   9   10   11